Iceland imewashangaza England baada ya kuwatungua kwa bao 2-1 kwenye mchezo wa hatua ya 16 bora ya michuano fainali za mataifa ya Ulaya kipigo ambacho kinaikumbusha England mwaka 1950 iliponyukwa na Marekani kwenye michuano ya kombe la dunia iliyofanyika Brazil.
England imeabishwa na timu inayotoka kwenye taifa lenye wakazi wasiozidi 330,000 huku ikiwa nafasi ya 34 kwenye viwango vya FIFA licha ya England kutangulia kwa bao la mkwaju wa penati uliofungwa na Wayne Rooney.
Iceland walisawazisha bao hilo baada ya dakika moja baadaye baada ya walinzi wa England kushindwa kudhibiti mpira mrefu wa kurushwa uliomkuta Ragnar Sigurdsson ambaye aliukwamisha kwenye neti kwa shuti la karibu.
Kiwango kibovu kilichooneshwa na England kilizidi kuwatia aibu baada ya Kolbeinn Sigthorsson kupachika bao lililoipa ushindi Iceland.
Hodgson alifanya mabadiliko lakini haikusaidia mbele ya Iceland wambao hawakupewa nafasi ya kupenya mbele ya England kabla ya filimbi ya mwisho kupulizwa.

Post a Comment

 
Top