Baada ya Hospitali ya
Taifa Muhimbili Dar es salaam kuja na mapendekezo ya kuboresha huduma za
chakula kwa wagonjwa wote watakaolazwa kuanzia Julai Mosi mwaka huu ili
kuwaondolea ndugu wa wagonjwa usumbufu na gharama za usafiri wakati
wanapokwenda kuwaona ndugu zao.
Leo June 25 2016 Waziri
wa afya, Maendele ya jamii, jinsia, wazee na watoto, Ummy
Mwalimu mbele ya waandishi wa habari ameagiza kusitishwa kwa muda zoezi hilo
mpaka hapo Wizara itakapopata taarifa za kutosha kuhusu faida na hasara za
utaratibu mpya unaopendekezwa, Waziri Mwalimu amesema……..
***’Hata hivyo
nimepokea maoni mengi kutoka kwa wananchi na wadau mbalimbali kuhusiana na
hatua iliyochukuliwa na Hospitali ya Taifa Muhimbili, ambapo itaanzisha
utaratibu utakaowezesha wagonjwa kuchangia gharama ya chakula ili chakula
kiweze kuandaliwa na hospitali badala ya utaratibu wa sasa’
***’kufuatia hali hii kuleta wasiwasi kwa wananchi na
wagonjwa, nimeagiza Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kusitisha utaratibu huo mpak
hapo tutakapopata taarifa za kutosha kuhusu faida na hasara za utaratibu mpya
unaopendekezwa’:-Waziri Ummy Mwalimu
Post a Comment