Umoja wa Mataifa unasema, nchi za
Afrika Kusini ya Sahara, zinapata hasara ya dola kama bilioni 95 kila
mwaka, kwa sababu ya tafauti baina ya wanaume na wanawake.
Mkuu wa
Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa, Helen Clark, anasema katika
sehemu nyingi za Afrika, wanawake wanapata tabu kukopa fedha, kwa sababu
hawana ardhi ya kuweka dhamana.Hii inamaanisha hawawezi kununua mbegu nzuri na mbolea, na kwa hivyo hawawezi kuzalisha mazao kwa wingi.
Bi Clark anasema, tofauti zikiondolewa, basi uchumi wa Afrika utakuwa kwa kiwango kikubwa zaidi.
No comments:
Post a Comment