Waziri wa Elimu Joyce Ndalichako amesema wanafunzi wote wanaosoma vyuo
vikuu wasio na sifa wataondolewa bila kujali wapo mwaka wa ngapi na hata
waliopo kazini wataondolewa kwa kuwa hao ndio wanatumia njia za mkato
kwenda kupata kazi japokuwa hawana sifa.
Waziri amevitaka vyuo vikuu kuchukua wanafunzi walio bora ili kuweka sifa ya ubora wa vyuo vyao
Na kuhusu vyuo vilivyochukua fedha ambazo hazikustahili vitalazimika
kurudisha fedha hizo na kisha kuchukuliwa sheria kwa waliohusika,
amesema bado wanaendelea kugundua idadi kubwa ya wanafunzi mfu
walioombewa fedha tangia waanze zoezi hilo na sasa wamefikia vyuo vitatu
tu.
BOFYA HAPA KUTAZAMA VIDEO KMAILI
No comments:
Post a Comment