Ugiriki yapendekeza mageuzi ya uchumi





Mapendekezo mapya yanatarjiwa kupigiwa kura bungeni

Masoko ya hisa ya Ulaya yamepanda kufuatia pendekezo la hivi karibuni lililowasilishwa na Ugiriki kwa wakopeshaji wake.
Mipango hiyo iliwasilishwa na serikali Athens Alhamisi usiku kwa matumaini ya kupata mkopo mpya kukwepa kufilisika.
Mageuzi hayo yanakaribiana na wanayotafuta wakuu wa shirika la fedha la kimataifa IMF, Umoja wa Ulaya na benki kuu ya Ulaya -- wanaojadili mpango huo kupitia njia ya simu.
Bunge la Ugiriki linatarajiwa kupigia mapendekezo hayo kura.
Lakini licha ya yatakayofikiwa, waziri mkuu wa Ugiriki, Alexis Tsipras anaonekana kurudi nyuma.
Hatua alizokubali zinaambatana na kupandisha kodi, kupunguza mishahara ya wafanyakazi wa umma na kuzidisha ubinfasishaji.




null
Wananchi wengi wanajaribu kutoa fedha katika mabenki Ugiriki

Yote yakia ni baadhi ya yanayopendekezwa na wakopeshaji wa Ugiriki.
Kwahivyo kura ya maoni ilikuwa na maana gani?
Kwa kiwango fulani ni suala la sifa ya nchi, lakini taifa hilo limejivunia kutofuata maagizo.
Viongozi wakuu wa chama cha Syriza wanasema kilinufaika kwa kuimarisha msimamo wa waziri mkuu huyo katika kuidhinisha hatua.
Hata hivyo hilo halikuja bure, yameakuwa na athari kama benki kufungwa, kurudi kwa mfumko wa bei na kuidhinisha uhusiano mbaya na Umoja wa Ulaya.
Mapendekezo hayo huenda yakapita bungeni lakini kutakuwa na shutuma nyingi nyumbani.

Post a Comment

 
Top