Friday, 24 July 2015

KIPI UNAJIFUNZA KUTOKA KWAO

     Natumaini unachochakujifunza kutoka kwao kwanzia mavazi muonekano wao wa kipindi hicho na sasa.Ama kweli hata mbuyu ulianza kama mchicha,leo hii jamaa hawa wamekua mfano mkubwa tena unaotamaniwa na kila mmoja wa watu wenye kuhitaji kufikia level walzofika kwa sasa.
       Lakini tambua mafanikio hayaji kwa kukaa kijiwni nakupanga mikakati mingi bila vitndo.Kama kijana ni lazima ujitume katika kiloa jambo unalolifanya ili kuweza kutimiza malengo yako.Epuka kutumia muda wako katika mambo yasiyo ya maendleo.Jitahidi kila siku kufanya jambo jipya katika misha yako juu ya ndoto zako.Usiwe na tamaa ya mafanikio ya ghafla maana uatakata tamaa pindi utakaposhindwa.Jaribu kuweka malengo yako na namna ya kuyafikia na ujitahidi sana kusimamia sheria zako ulizojiwekea juu ya malengo yako.
Ukiwa kama kijana mwenye nguvu na utashi hupaswi kukata tamaa katika mambo yanayohusu maendeleo hususani malengo yako.Kaa mbali na vishawishio na watu wavivu maana hao ndio maadui wakubwa wa\ maendeleo ya taifa letu.

No comments:

Post a Comment