Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar
es Salaam, Kamishna wa Polisi (CP), Simon Sirro akizungumza katika
mkutano na waandishi wa habari ofisini kwake Dar es Salaam leo, wakati
akitangaza kiama kwa mwananchi yeyote atakayefanya maandamano Septemba
Mosi ya kupinga udikiteta Tanzania yaliyoandaliwa na Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (Chadema).
Kamanda Sirro akisisitiza jambo kwenye mkutano huo.
Magari ya polisi yenye zaidi ya askari
80 yakiondoka Kituo cha Polisi cha Kati, yakielekea Vikindu kwa ajili ya
Operesheni saka majambazi.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Askari wa kikosi maalumu cha kupambana
na uhalifu wakiondoka Kituo Kikuu cha Polisi cha Kati kuelekea Vikindu
kwa operesheni maalumu ya kuwasaka watu wanaotuhumiwa kwa ujambazi.
Na Dotto Mwaibale
KAMANDA wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar
es Salaam, Kamishna wa Polisi (CP), Simon Sirro ametangaza kiama kwa
mwananchi yeyote atakayefanya maandamano Septemba Mosi ya kupinga
udikiteta Tanzania yaliyoandaliwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(Chadema)
“Jeshi la polisi mkoa wa Dar es Salaam
tumejipanga vizuri siku hiyo nawaomba wananchi wasidhubuti kujitokeza
kuandamana siku hiyo kwani watakiona cha moto” alisema CP Sirro.
Sirro alisema tayari jeshi hilo lina
taarifa za kiinteligensia kuwa kuna vijana wanapewa fedha kwa ajili ya
kuandamana na kufanya fujo Septemba mosi.
Aliwasihi wananchi hasa vijana kutoingia barabarani Septemba mosi na kuwaachia wachache wenye nia ya kuletafujo.
“Ni rai yangu wale wananchi wazalendo
wan chi hii wasiopenda kupambana na jeshi lao la polisi ambalo
linawalinda na kulinda mali zao siku hiyo wasiingie barabarani,”
alisema.
Aliwakaribisha wanao taka kuingia
barabarani na kupambana na jeshi hilo na kuwa watakamatwa na kufikishwa
kwenye mkono wa sheria.
“Sisi tupo vizuri na tupo imara hasa kwa
wale wanaopenda kuvunja sheria kwa makusudi wata wajibika kwa mujibu wa
sheria, hivyo suala la utiiwa sheria bila shuruti ni la msingi sana,”
alisema Sirro.
Alisema jeshi hilo limejiandaa kwa
wananchi wachache ambapo alibainisha wananchi wengine hawana haja na
maandamano hayo huku akibainisha vijana wachache wenye shida kupewa
fedha na viongozi kwa lengo la kuandamana.
“Jiulize hiyo 40,000 unayo pewa kuingia
barabarani na matokeo yake ukavunji kama mguu hiyo 40,000 ina thamani
gani kwani… kwa hiyo mimi kama kiongozi wenu wa jeshi la polisi na
sisitiza na ninaelekeza tuwaache wale wenye sababu zao binafsi waingie
barabarani,” alisema.
Katika hatua nyingine Kamanda Sirro
alisema askari zaidi ya 80 wa kikosi maalumu cha kupambana na uhalifu
wameondoka kwenda vikindu na maeneo mengine wilayani Mkuranga mkoani
Pwani kufanya operesheni ya kuwasaka watu wanaodhaniwa kujihusisha na
ujambazi.
Post a Comment