Tuesday, 16 August 2016

Dr KIGWANGALA ASHTUKIA SHIRIKA LILILOKUWA LIKICHOCHEA MAPENZI YA JINSIA MOJA

Yabainika walikuwa na mradi wa kuhamasisha mapenzi ya jinsia moja ukifadhiliwa na JHPIEGO

- Baadhi ya watendaji wa Asasi hiyo walikuwa kwenye asasi iliyofutiwa usajili ya "Sisi kwa Sisi"


Dkt. Kigwangalla, Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, jinsia, wazee na watoto Na Mbunge wa Jimbo la Nzega Vijijini, Leo jioni ameendesha Operesheni Maalum ya ukaguzi wa ofisi za shirika lisilo la kiserikali la Community Health Education Services and Advocacy (CHESA), ikiwa ni muendelezo wa vita ya uhamasishaji wa vitendo Vya mapenzi ya jinsia moja ulioanza kuota mizizi nchini.







Shirika la CHESA, pamoja na Mashirika mengine (sintoyataja hapa) yanasemwa kuwa yanaendesha shughuli ambazo hayakusajiliwa kufanya, ikiwemo tuhuma za kuhamasisha watu wanaofanya mapenzi ya jinsia moja kudai haki zao kupitia miradi yao na harakati nyingine mbalimbali.

Mashaka yametanda kwenye nchi nyingi Afrika, dunia ya waarabu na nchi zenye wakristo wa Katoliki kuhusiana na marafiki zetu wanaoruhusu mambo haya kwenye sheria, mila na desturi zao kuanzisha mikakati ya kichini chini ya kusambaza pesa kwenye vikundi mbalimbali vya kijamii na asasi zisizo za kiserikali ili kuwahudumia, kuwaunga mkono, kuwaunganisha, kuwatetea, kuwalinda, kuwawezesha, na kuhamasisha jitihada za siri sana na makini za kueneza mapenzi ya jinsia moja nchini. Pia kuhalalisha kama utamaduni Mpya kwa kisingizio cha "Haki za binadamu".

Tanzania imesaini International Bill of Rights (mkataba wa kimataifa wa Haki za binadamu) lakini kwenye mkataba huo Hakuna kipengele hata kimoja kinachoelezea uwepo wa Haki zinazodaiwa na kundi hili.

ImageUploadedByJamiiForums1471287494.537030.jpg


"Serikali itaendesha harakati nzito za uchunguzi wa pesa zote zinazoenda kwenye NGOs Na vikundi mbalimbali na kufuatilia pesa hizo zimeenda kufanya nini kwenye jamii," alisema Dkt. Kigwangalla.



"Nimewapa agizo wataalamu kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kushirikiana na jeshi letu la polisi kufanya kazi hiyo na kuyafikisha mahakamani Mashirika yote yatakayokutwa na hatia na pia kuchukua hatua ya kuyafutia usajili mashirika yote yatakayobainika kukiuka masharti ya usajili wao kwa mujibu wa sheria. Kwa mfano, 'coincidentally', tayari shirika hili litapaswa kutoa maelezo juu ya pesa lilizopokea kutoka shirika la kimataifa la JHPIEGO kutekeleza mradi wa SAUTI, ambao kwenye taarifa zake za mwaka limezificha. Mradi wa SAUTI unahudumia watu wanaofanya mapenzi ya jinsia moja" aliendelea kusema Dkt. Kigwangalla.

ImageUploadedByJamiiForums1471287450.147265.jpg

Shirika la CHESA kwenye usajili wake hakuna mahali linaeleza kwenye Katiba inayolianzisha kuwa litatoa huduma hizo. Na sababu ni rahisi, kwamba lisingeweka huduma hizo Kwa kuwa lisingesajiliwa.

Miaka ya hivi karibuni Serikali ilifuta usajili wa NGO moja iliyojulikana kama 'Sisi Kwa Sisi' Kwa tuhuma kama hizi. Kwenye uchunguzi huu, imebainika kuwa baadhi ya viongozi wa iliyokuwa Sisi Kwa Sisi ni waandamizi kwenye CHESA. Je, Sisi Kwa Sisi Siyo CHESA kwenye rangi nyingine?

No comments:

Post a Comment