Ujerumani yawekeza dola milioni 320 Tanzania


Serikali ya Ujerumani imewekeza nchini jumla ya miradi 8 yenye thamani ya dola za kimarekani millioni 320 katika sekta ya afya, nishati, ujenzi na uzalishaji wa bidhaa mbalimbali.

Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania Dirk Smelty
Akiongea na waandishi wa habari hii leo jijini Dar es salaam, mkurugenzi wa biashara na uwekezaji wa Ujerumani nchini Tanzania, Dirk Smelty amesema, nchi hiyo imeona nia ya kuisaidia Tanzania kuondokana na bidhaa zisizo na ubora.
Pia kutatua changamoto mbalimbali zinazorudisha nyuma juhudi za ukuaji kiuchumi hususani sekta ya ujenzi wa nyumba na barabara, uhaba wa vifaa tiba na dawa sambamba na uuzaji wa vifaa vya umeme jua maeneo ya vijijini.
Naye afisa habari wa ubalozi wa ujerumani bwana John Merinikon amesema kuwa nchi hiyo imeona nia ya kuwekeza tena nchini kwa kasi kubwa baada ya miaka 20 kutokana na serikali iliyopo madarakani kuonesha nia ya kupambana na ufisadi, kuongeza uwazi na uzalishaji wa viwanda

Post a Comment

 
Top