Monday, 4 July 2016

ICELAND YATOLEWA NA UFARANSA MICHUANO YA EURO

 Dimitri Payet akibusu kiatu cha Antonie Griezmann baada ya kufunga bao


 Iceland wameondoka katika Euro lakini kwa hakika watabaki katika vinywa vya wapenzi wa Soka. Nahodha wao Aron Gunnarsson amesema kwa hakika huu ni mwanzo wao wa kuanza kukwea jukwaa la kimataifa.
Anasema kile walichokipata jana katika Stade de France kimewasikitisha lakini wanajivunia ushiriki wao kwani umewajenga sana.
Sasa wanajipanga katika kuwania kufuzu kushiriki kwa mara ya kwanza katika kombe la Dunia litakalofanyika Urusi mwaka 2018 wakiwa kwenye kundi ambalo lina Croatia, Ukraine, Finland, Uturuki na Kosovo.
Inakadiriwa asilimia 10 ya Raia wote wa nchi walikuwa wamesafiri kuja kuishabikia timu yao.
Michuano hii pia imetumika kuwatangaza wachezaji na sasa tutaanza kukona wakienda huku na kule, kwa mfano mshambuliaji Hal Robson Kanu wa Wales ambaye ameachwa huru na Reading mwishoni mwa msimu wa 2015-16 hivi sasa ameanza kutakiwa huku na kule na hasa baada ya bao lake lile alilogeuka katika kumi na nane akawabamiza ubelgiji na kuipeleka Wales nusu fainali

No comments:

Post a Comment