Kampini ya Apple kununua Tidal ya Jay Z

 Kanye West na Jay Z
Kampuni ya Apple inadaiwa kutaka kuchukua umiliki wa huduma ya kusikiliza muziki ya moja kwa moja ya mwanamuziki Jay Z Tidal.
Kampuni hiyo imeripotiwa kwamba inaangazia wazo la kuinunua huduma hiyo kutokana na ushirikiano wake na wanamuzika bingwa kama vile Kanye West na Madonna.
Duru zimearifu jarida la Wall Street kwamba mazungumzo yameanza na huenda yakasababisha kupatikana kwa makubaliano.

Msemaji wa Tidal amekana kwamba imefanya mazungumzo na Apple.
Jay Z alizindua huduma hiyo mnamo mwezi Machi mwaka uliopita kama mpinzani wa Spotify.
Kampuni ya kiteknolojia ya Sweden, Aspiro ambayo ilikuwa ikiimiliki Tidal,ilinunuliwa na mwanamuziki huyo wa mtindo wa Rap kwa takriban dola milioni 56.
Jay Z aliandamana na Kanye West.
Alicia Keys na mkewe Beyonce ambao wote ni wadau katika kampuni hiyo.

Post a Comment

 
Top