Saturday, 25 June 2016

TAMKO LA WAZIRI UMMY MWALIMU JUU YA SWALA LA KUWAHUDUMIA CHAKULA WAGONJWA MUHIMBILI



Baada ya Hospitali ya Taifa Muhimbili Dar es salaam kuja na mapendekezo ya kuboresha huduma za chakula kwa wagonjwa wote watakaolazwa kuanzia Julai Mosi mwaka huu ili kuwaondolea ndugu wa wagonjwa usumbufu na gharama za usafiri wakati wanapokwenda kuwaona ndugu zao.
Leo June 25 2016 Waziri wa afya, Maendele ya jamii, jinsia, wazee na watoto, Ummy Mwalimu mbele ya waandishi wa habari ameagiza kusitishwa kwa muda zoezi hilo mpaka hapo Wizara itakapopata taarifa za kutosha kuhusu faida na hasara za utaratibu mpya unaopendekezwa, Waziri Mwalimu amesema……..
***’Hata hivyo nimepokea maoni mengi kutoka kwa wananchi na wadau mbalimbali kuhusiana na hatua iliyochukuliwa na Hospitali ya Taifa Muhimbili, ambapo itaanzisha utaratibu utakaowezesha wagonjwa kuchangia gharama ya chakula ili chakula kiweze kuandaliwa na hospitali badala ya utaratibu wa sasa’
***’kufuatia hali hii kuleta wasiwasi kwa wananchi na wagonjwa, nimeagiza Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kusitisha utaratibu huo mpak hapo tutakapopata taarifa za kutosha kuhusu faida na hasara za utaratibu mpya unaopendekezwa’:-Waziri Ummy Mwalimu

No comments:

Post a Comment