Baada ya kukosa penati na Argentina
kushindwa kutwaa kombe la Copa America, mchezaji nyota Lionel Messi
amechukua uamuzi mgumu wa kujiuzulu kuichezea tena timu ya taifa.
Ni kwa miaka tisa mfululizo
Argentina imejikuta ikipoteza nafasi ya kutwa kombe mara nne katika
michuano ya kimataifa, huku Messi akishindwa kuisaidia kabisa.
Messi akiwa na Argentina amefanikiwa
mara moja tu kutwaa medali ya dhahabu katika michuano ya Olimpiki.
Lakini akiwa na klabu yake ya
Barcelona Messi ameshinda ubingwa wa Ligi ya Kuu ya Hispania 'La
Liga' mara nane na Ligi ya Mabingwa Ulaya mara nne.
Lionel Messi akipiga mkwaju wa penati aliyoikosa na kuamua kufanya maamuzi magumu.
No comments:
Post a Comment