Miamba ya soka la Ujerumani Bayern Munich wametwaa ubingwa wa michuano ya Audi mwaka 2015.
Bayern wakicheza katika uwanja wao Allianz Arena Jijini Munich, wameibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya klabu ya Real Madrid ya Hispania.Bao la ushindi la Bayern lilifungwa Dakika ya 88 na mshambuliaji Robert Lewandowski,alieunganisha mpira wa adhabu uliopigwa na Douglas Costa.
Katika mchezo wa kumsaka mshindi wa tatu Tottenham Hotspur waliwachapa AC Milan kwa mabao 2-0 kwa mabao ya Nacer Chadli, Dakika ya 8, na Thomas Carroll, Dakika ya 71.
No comments:
Post a Comment