Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki-moon, amesema amemfukuza mkuu wa kulinda amani toka UN nchini Afrika ya kati baada ya kutuhumiwa kuhusika na madai ya unyanyasaji wa watoto kingono.
Bwana Ban amesema mwanadiplomasia wa Senegal Babacar Gaye angeachia ngazi kama mkuu wa ujumbe. Ban aliongeza kuwa alipatwa na hasira na aibu baada ya taarifa hizo za unyanyasaji wa ngono na ukandamizaji kwa watoto.
Taasisi ya kutetea haki za binaadam Amnesty International imewatuhumu wanajeshi hao wa kulinda amani wa UN kwa kumbaka msichana wa miaka kumi na miwili na kumuua kijana na baba yake katika mji mkuu wa nchi hiyo Bangui, mapema mwezi huu.
Uchunguzi pia unaendelea namna wanajeshi hao wa umoja wa mataifa kuhusika na madai ya unyanyasaji dhidi ya wanajeshi wa Ufaransa mwaka jana.
Post a Comment