Sunday, 30 August 2015

Wahamiaji : nchi za ulaya zakosolewa

         Laurent Fabius
Waziri wa mashauri ya kigeni nchini Ufaransa Laurent Fabius ameelezea hisia za baadhi ya nchi za ulaya dhidi ya suala la uhamiji kuwa sawa na sakata.
Amezilaumu nchi za ulaya hasusan zilizo mashariki mwa ulaya kwa kukataa kuwaruhusu wahamiaji.
 
Wahamiaji kwenye mpaka wa Hungary na Serbia
Bwana Fabius aliiilaumu Hungary kwq kujenga ua ulio na lengo la kuzuia watu wanaowasili wakipitia nchini Serbia akisema kuwa hatua hiyo haiendi sawa na maadili ya ulaya.
Ufaransa imejiunga na Uingezea pamoja na na Ujerumani katika kuitisha mkutano wa dharura na mawaziri wa nchi za ulaya kutafuta njia za kukabiliana idadi ya wahamiaji inayozidi kuongezeka.

Wednesday, 26 August 2015

Salva Kiir atia saini mkataba wa amani


             
  Salva Kiir
Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir ametia saini makubaliano ya amani yanayonuiwa kumaliza mzozo uliodumu kwa muda wa miezi ishirini.
Bwana Kiir, ambaye alikataa kutia saini mkataba huo wiki iliyopita amesema bado hana imani kamili kuhusu mkataba huo.
Usitishwaji wa mapigano unapaswa kutekelezwa katika muda wa saa 24 na majeshi ya kigeni yanapaswa kuondoka nchini humo.

Hakuna wanajeshi watakaoruhusiwa kufika karibu na mji mkuu Juba.
Kiir ambaye alikabiliwa na shinikizo za kimataifa kuidhinisha mkataba huo anatarajiwa kuunda serikali ya umoja wa kitaifa na kiongozi wa waasi Riek Machar.

Thursday, 13 August 2015

Watu 60 wameuawa Baghdad





Watu 30 wameuawa Baghdad kufuatia bomu kubwa lililotegwa ndani ya lori

Mlipuko mkubwa kutoka kwa lori lililokuwa limeegezwa katika mji mkuu wa Iraq, Baghdad umesababisha vifo vya zaidi ya watu 60.
Maafisa walisema kuwa gari lililokuwa na mtambo wa kutengeneza barafu lililipuka Kaskazini Mashariki mwa jiji hilo.
Mlipuko huo ulitokea katika eneo la soko lililo na watu wengi karibu na Wilaya inayokaliwa zaidi ya Washia ya Sadri.




Hakuna kundi lolote lilolodai kuhusiana na mlipuko huo.

Hakuna kundi lolote lilolodai kuhusiana na mlipuko huo.
Wapiganaji wa kundi la Waislamu wenye itikadi kali hushambulia maeneo yanayokaliwa na Washia mara nyingi.

Ban Ki moon afanya maamuzi magumu



Babacar Gaye

Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki-moon, amesema amemfukuza mkuu wa kulinda amani toka UN nchini Afrika ya kati baada ya kutuhumiwa kuhusika na madai ya unyanyasaji wa watoto kingono.
Bwana Ban amesema mwanadiplomasia wa Senegal Babacar Gaye angeachia ngazi kama mkuu wa ujumbe. Ban aliongeza kuwa alipatwa na hasira na aibu baada ya taarifa hizo za unyanyasaji wa ngono na ukandamizaji kwa watoto.
Taasisi ya kutetea haki za binaadam Amnesty International imewatuhumu wanajeshi hao wa kulinda amani wa UN kwa kumbaka msichana wa miaka kumi na miwili na kumuua kijana na baba yake katika mji mkuu wa nchi hiyo Bangui, mapema mwezi huu.
Uchunguzi pia unaendelea namna wanajeshi hao wa umoja wa mataifa kuhusika na madai ya unyanyasaji dhidi ya wanajeshi wa Ufaransa mwaka jana.

Thursday, 6 August 2015

Je unataka kuishi maisha marefu duniani ?

   


Ukila vyakula vilivyotiwa viungo kila siku unajiongezea maisha marefu; 'Utafiti'

Je unataka kuishi maisha marefu duniani ?
Utafiti mmoja uliofanywa nchini China umebaini kuwa ukila chakula kilichotiwa viungo kila siku unajiongezea maisha marefu.
Utafiti huo haswa umeonesha kuwa ukila chakula hususan pilipili utaishi maisha marefu zaidi duniani.
Watafiti mjini Baijing walidadisi maisha na vyakula wanavyokula wenyeji nusu milioni katika kipindi cha utafiti cha miaka 7.
Utafiti huo ulibaini kuwa wale waliokula chakula kilichojumuisha pilipili walikuwa katika hali bora zaidi kiafya wala hawakuwa katika hatari ya kuaga dunia.
Hali yao ya siha ilitofautiana sana ikilinganishwa na wale ambao waliweka viungo katika vyakula vyao chini ya siku moja kwa juma .

Kiungo kinachopatikana katika pilipili, 'capsaicin' kinauwezo wa kupigana na seli zinazofanya mtu azeeke
Watafiti hao walitoa tahadhari.
Wanasema kuwa utafiti huo ulikuwa wa ushahidi tu lakini wakashauri utafiti zaidi ufanyika kwengineko ilikutilia pondo utafiti wao.
Hata hivyo walibaini kwa uhakika kuwa kiungo kinachopatikana katika pilipili, 'capsaicin' kinauwezo wa kupigana na seli zinazotuma ujumbe kwa ubongo kuwa mtu amezeeka na kusababisha viashiria vya utu uzima.

Je ni msanii yupi anayelipwa pesa nyingi zaidi ?



Msanii anayelipwa pesa mshahara mkubwa zaidi duniani Robert Downey Jr - $80m

Usanii wa uigizaji katika filamu hutuacha na hisia tofuati tunapowatazama hasusan waigizaji nguli.
Lakini je, unafahamu kiasi cha fedha wanazolipwa kwa uigizaji wao ?
Jarida la Forbes limezindua orodha ya waigizaji bora na wanaolipwa mshahara wa juu zaidi duniani.


Msanii Jackie Chan wa filamu ya Karate Kid miongoni mwa nyingine nyingi tu, ameorodheshwa katika nafasi ya pili.
Jarida hilo limeangazia faida wanazopata baada ya kulipa gharama kama vile kodi na ada ya wasimmamizi wao.
Kwa mwaka wa tatu mfululizo, muigizaji wa filamu ya Iron Man, Robert Downey Jr anaongoza orodha hiyo.
Downey Jr alitia kibindoni dola milioni $80m .
Downey ameshiriki katika filamu za 'Avengers' na 'Age of Ultron'.
Na kwa mara ya kwanza, orodha hiyo imewashirikisha waigizaji wanaoigiza nje ya Hollywood.


Bradley Cooper ameorodheshwa katika nafasi ya 4 - $41.5m
Hii inamaanisha kuwa wasanii watajika katika filamu nje ya Marekani kama vile Bollywood ya India na wasanii wa Asia pia wamejumuishwa katika orodha hiyo.
Muigizaji nyota kutoka Uingereza Daniel Craig aliorodheshwa katika nafasi ya 15 sawa na Chris Hemsworth kutoka Australia.
Wawili hao walizoa takriban dola milioni $27m kwa mujibu wa Forbes.
Msanii Jackie Chan wa filamu ya Karate Kid miongoni mwa nyingine nyingi tu, ameorodheshwa katika nafasi ya pili.


Tom Cruise ameorodheshwa katika nafasi ya 6- $40m
Chan alipokea dola milioni 50 mwaka uliopita kwa kazi yake.
Tazama Orodha kamili hapa
Hawa ndio wasanii wanaolipwa vyema kulingana na Forbes.
1. Robert Downey Jr - $80m
2. Jackie Chan - $50m
3. Vin Diesel - $47m
4. Bradley Cooper - $41.5m
5. Adam Sandler - $41m
6. Tom Cruise - $40m
7. Amitabh Bachchan - $33.5m
8. Salman Khan - $33.5m
9. Akshay Kumar - $32.5m
10. Mark Wahlberg - $32m

Bayern Munich mabingwa wa Audi

    



Kikosi cha Bayern munich

Miamba ya soka la Ujerumani Bayern Munich wametwaa ubingwa wa michuano ya Audi mwaka 2015.
Bayern wakicheza katika uwanja wao Allianz Arena Jijini Munich, wameibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya klabu ya Real Madrid ya Hispania.
Bao la ushindi la Bayern lilifungwa Dakika ya 88 na mshambuliaji Robert Lewandowski,alieunganisha mpira wa adhabu uliopigwa na Douglas Costa.
Katika mchezo wa kumsaka mshindi wa tatu Tottenham Hotspur waliwachapa AC Milan kwa mabao 2-0 kwa mabao ya Nacer Chadli, Dakika ya 8, na Thomas Carroll, Dakika ya 71.

Uzinduzi wa Windows 10 ni mwanzo mpya



Windows 10

Programu ya Windows 10 imeadhimisha mwanzo mpya katika kompyuta za kibinafsi ,kulingana na mtendaji mkuu wa kampuni ya Microsoft .
Programu hiyo ilizinduliwa kimataifa siku ya Jumatano, na ni jaribio la kampuni hiyo kujaribu bahati yake katika sekta ya simu.
Windows 10 itatolewa bure kwa wateja wengi kama hatua ya kuboresha programu hiyo.


Windows 1 hadi 10
Hata hivyo makampuni yatalazimka kulipia toleo hilo jipya hivyo watengenezaji wa PC watahitajika kuiweka katika vifaa hivyo.
Wachambuzi wanasema mkakati huo umezinduliwa ili kuharakisha utumizi wake.
Alipofanya mazungumzo ya kipekee na BBC, Satya Nadella alisema ''programu ya windows 10 ni hatua kubwa kwetu sisi kama kampuni, na katika sekta nzima''.


Windows 10
Microsoft imekua mbioni kuizindua kwa muda wa wiki kadhaa zilizopita, hivyo si kila mtu atapata fursa hiyo ya kuboreshewa siku ya kuanzishwa kwake.

Fiorentina yaichapa Chelsea kwao


 
 Kocha wa Chelsea Jose Mourinho

Klabu ya soka ya Fiorentiana ya Italia imewachapa mabingwa wa ligi ya England Chelsea kwa bao 1-0.
Bao pekee la ushindi la Fiorentina ama maarufu kama Viola liliwekwa kimiani na beki Gonzalo Rodríguez raia wa Argentina katika Dakika ya 34 baada ya Kipa wa Chelsea Begovic kutema Shuti la Alonso Mendoza.
Mchezo huu ni wa mwisho wa kirafiki kwa klabu ya Chelsea inayonolewa na Kocha Jose Mournho kabla ya kuanza kwa kipute cha ligi kuu ya Engalnd hapo Augusti 8.
Ambapo wataanza utetezi wa ubingwa wao kwa kucheza Mechi yao ya kwanza dhidi ya timu ya Swansea City.

Wasifu wa Edward Lowassa

  



Je unamfahamu Edward Lowassa ni nani katika siasa za Tanzania ?

Umoja usio rasmi wa vyama vinne vya upinzani nchini Tanzania unajulikana kwa jina la Katiba ya Wananchi (UKAWA), baada ya kusubiri kwa muda hatimaye umemtangaza Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa kuwa mgombea wake wa urais.
Lowassa anagombea kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), huku vyama vingine vitatu vikimuunga mkono. Hii inatokana na sheria za Tanzania ambayo haitambui umoja wa vyama.
Kabla ya kujiengua chama Tawala chama cha Mapinduzi CCM, Edward Lowassa amekuwa mwanachama wa CCM kwa muda wa miaka 38, ambapo alijiunga na chama hicho mara tu baada ya kumaliza elimu yake ya chuo kikuu mwaka 1977.
Hatua ya mwanasiasa huyo mashuhuri nchini Tanzania kuamua kujiunga na chama cha upinzani Chadema, ikiwa imebaki miezi mitatu tu kuelekea uchaguzi mkuu, kumebadilisha kabisa upepo wa kisiasa nchini Tanzania, na hasa uchaguzi mkuu ujao.


Wasifu wa Lowassa
Lowassa alikuwa Maziri Mkuu kati ya mwaka 2005 na 2008 kabla ya kujiuzuLu wadhifa huo kufuatia sakata la kashfa ya rushwa iliyohusisha kampuni ya kuzalisha umeme ya ki-Marekani Richmond Development Company LLC ya Houston Texas.
Hata hivyo wakati anatangaza kuhamia kwake Chadema, Lowassa alikanusha katu katu kuhusika kwa namna yoyote na kashfa hiyo na kudai kuwa yeye alifuata tu amri kutoka kwa ‘wakubwa’ walio juu yake.
“Kama kuna mtu yeyote mwenye ushahidi basi na aende mahakamani ama sivyo anyamaze” alisema Lowassa


“Kama kuna mtu yeyote mwenye ushahidi basi na aende mahakamani ama sivyo anyamaze” alisema Lowassa
Kuhama kwake kunamfanya Lowassa kuwa ndie kiongozi wa kwanza wa ngazi ya juu kabisa wa CCM kukihama chama hicho tangu kuanza kwa mfumo wa vyama vingi nchini Tanzania mnamo mwaka 1992.
Mwanajeshi wa zamani na aliyewahi kupigana wa vita kati ya Uganda na Tanzania mwaka 1978/79, Lowassa aliiambia hadhara kwamba akiwa kama mtu mwenye uchungu na nchi yake isingekuwa rahisi kubaki ndani ya CCM huku akiona chama hicho kimepoteza mwelekeo na sifa ya kuongoza nchi.
Lowassa amekimbilia upinzani baada jina lake kukatwa wakati alipoomba kuwa mgombea urais kupitia chama tawala CCM katika uchaguzi mkuu ujao utakafanyika mwezi Oktoba mwaka huu.
Wakati mchakato wa CCM wa kumtafuta mgombea wao wa urais ulipoanza, Lowassa ndiye aliyekuwa kinara wa wagombea wote 42. Kila kona aliyozunguka, mikutano yake ya hadhara ilivutia maelfu ya watu waliomuunga mkono.
Wakati chama cha CCM kilimtaka kila mgombea apate sahihi za wadhamini 450 lakini Lowassa alipata sahihi za wadhamini zaidi ya 700,000.


Wasifu wa Edward Lowassa
Hata hivyo mchujo wa chama ulipofanyika jina lake lilikatwa mapema kabla hata ya kupelekwa kwenye vikao vya vya juu vya chama hicho. Ambapo baadae Waziri wa Ujenzi John Pombe Magufuli ndiye aliyeibuka kidedea na kuwa mgombea kupitia chama tawala CCM.
Lowassa ameushutumu mchakato CCM wa kutafuta mgombea urais akiuita kuwa ulijaa chuki na mizengwe dhidi yake, hali ambayo aliifananisha na ‘ubakaji wa demokrasia’
“Nitakuwa mnafki nikisema bado nina imani na CCM. CCM niliyoiona Dodoma si CCM niliyokulia”, alisema, na kuongeza “kama Watanzania hawapati maendeleo kupitia CCM basi wakayatafute nje ya CCM”
Wakati sakala la Richmond lilipoibuka miaka michache tu iliyopita, Chadema ilimfanya limsakama Lowassa kuwa ni mmoja wa mafisadi wakubwa nchini. Lakini wakati chama hicho kinamkaribisha kuwa mwanachama wao, kiligeuka na kusema hakuna mtu msafi nchini na kwamba hawawezi kuacha kumpokea mwanasiasa mwenye mtaji mkubwa wa wafuasi kama Lowassa.
Wakati akiwa Waziri Mkuu, Lowassa alisifika kama mchapakazi hodari na msimamiaji wa moja kwa moja wa shughuli za serikali. Bado anaendelea kufahamika kwa jina la utani la ‘mzee wa maamuzi magumu’.


Je unamfahamu Edward Lowassa ni nani katika siasa za Tanzania ?
Moja ya mafanikio makubwa ya uwaziri mkuu wake ni jitihada kubwa na mafanikio ya upatikanaji wa fedha za kujenga chuo kikuu cha Dodoma. Chuo hiki kikuu cha umma kilichopo katikati ya Tanzania kilianzishwa mwaka 2007.
Lowassa ni mashuhuri pia kwa kusimamia mpango wa serikali uliofanikiwa wa ujenzi wa shule za kata ambazo uliiletea Tanzania sifa kubwa kwa kutoa fursa ya watoto wengi kupata nafasi shuleni.
Mtoto wa Mzee Ngoyai Lowassa, ambaye aliwahi kuwa mtumishi wa serikali ya kikoloni, Lowassa ameanza harakati zake za kuwania urais tangu mwaka 1995 lakini inaarifiwa kwamba rais wa kwanza wa Tanzania Mwl Julius Nyerere alimkatalia kushika nafasi hiyo. Wafuasi wa Lowassa wamekuwa wakiyatupilia mbali madai hayo
Ulipofika uchaguzi wa mwaka 2005, Lowassa hakutaka kuwania urais, lakini badala yake alimnadi rafiki yake wa siku nyingi Rais wa sasa Jakaya Kikwete ambaye alipata ushindi wa kishindo wa zaidi ya asilimia 80.

Japan yakumbuka shambulio la Heroshima

 


Raia wa Japan wamefanya maombi leo

Raia wa Japan leo wanaadhimisha kumbukumbu ya miaka 70 tangu shambulio la kwanza la bomu la Atomiki kutekelezwa mjini Heroshima.
Takriban watu laki moja na arobaini walikadiriwa kupoteza maisha baada ya Ndege ya Marekani kudondosha bomu ambalo liliuharibu mji huo tarehe 6 mwezi Agosti mwaka 1945.
Watu elfu sabini walipoteza maisha papo hapo, huku wengine wa idadi kama hiyo walipoteza maisha kutokana na athari za mionzi ya sumu.
Katika hotuba yake, Waziri Mkuu wa Japan Shinzo Abe alisema kumbukumbu ya Heroshima inasisitiza uhitaji wa kufanya jitihada ya kupiga vita matumizi ya Nuklia.
Shambulio la Heroshima lilifuatiwa na shambulio jingine la bomu la Atomiki katika mji wa Nagasaki.
Japan ilijisalimisha siku kadhaa baadae, hatua iliyomaliza vita ya pili ya dunia

Hofu baada ya boti iliyojaa wahamiaji kuzama Libya


Hofu baada ya boti iliyojaa wahamiaji kuzama Libya

Waokoaji wanaendelea na shughuli ya kuwasaka mamia ya wahamiaji waliotumbukia baharini baada ya boti walimokuwa wakisafiria kwenda Ulaya kuzama majini katika bahari ya Mediterrania karibu na ufuo wa Libya.
Ripoti ambazo hazijathibitishwa zinasema kuwa takriban watu 700 walikuwa kwenye mtumbwi huo uliozama baada ya kukumbana na mawimbi makali.
Wanajeshi wa majini kutoka Ireland wanakisia kuwa idadi kubwa ya watu wamekufa maji.
Aidha shirika la madaktari wasiokuwa na mipaka Medecins Sans Frontieres (MSF) limeonya kuwa huenda kukazuka maafa makubwa kufuatia idadi kubwa ya abiria waliokuwa kwenye mtumbwi huo uliozama.
Inakisiwa kuwa takriban wahamiaji 2,000 walikufa maji kwanza mwanza wa mwaka huu wakijaribu kufika ulaya kupitia bahari hiyo ya Mediterranea
Meli nne za uokozi na ndege tatu zimetumwa huko kujaribu kunusuru maisha ya wahamiaji hao.

Takriban watu 700 walikuwa kwenye mtumbwi huo uliozama
Walinzi wa Ufuo wa bahari ya Uitaliano wamesema boti hiyo ya uvuvi iliyokuwa imebeba mamia ya wahamiaji.
Inavyoelekea boti hiyo ilikumbwa na dharuba lakini pia ilipenduka pale watu walipokurupuka upande mmoja walipoona chombo kingine kilichokuwa kikienda kuwasaidia.
Zaidi ya watu 150 wameokolewa lakini wengine wengi wanahofiwa wamekufa maji.
Msemaji wa shirika linalohusika na maswala ya wahamiaji IOM, Leonard Doyle ameiambia BBC kuwa
''Lazima tukumbuke kuwa hawa ni watu ambao hawajazoea usafiri wa baharini kwahivyo waliogopa.''
''Na wakati walipoona chombo kingine kinakuja kuwaokoa wakataharuki na kukurupuka upande mmoja''.

Zaidi ya watu 150 wameokolewa lakini wengine wengi wanahofiwa wamekufa maji.
Hilo ndilo tunalokariri kuwa hao walanguzi wa kusafirisha watu hawajali kabisa kuhusu maisha ya wahamiaji hao licha ya kuwa wamewalipa pesa nyingi kwa safari hizo hatari''.
Kwamba mkasa wa aina hii unaweza kutokea wakati ambao hata watu wamepelekewa chombo cha kuwaokoa karibu yao ni jambo la kusikitisha sana