Nimeona ni vyema kumkumbusha kila msosamji wa blog hii jambo hili,kwani watu wengi hususani wenye mafanikio makubwa aidha kielimu,kiuchumi,kisiasa,kimichezo nk,wamegubikwa na wimbi kubwa la lawama kwamba wamesahau walipotoka.Yawekana ni kweli kwamba watu wengi wanapopata mafanikio makubwa wanalewa kabisa na kuwapotezea ndugu na jamaa waliokua mchango mkubwa kipindi cha msoto.


 Kama wewe ni mmoja wa watu wanaotupiwa lawama kwamba wamsahau walipotoka basi badilika na ujaribu kukumbuka japo kiduchu ulikotoka.Waheshimiwa wengi hususani wabunge wamekuwa mfano mkubwa wakusahau walikotoka mara tu wanapopata ushindi katika uchaguzi.Waheshimiwa hawa husepa na kutokomea mijini na kuwaacha wananchi wao katika msoto mkali na wao wakila raha na mema ya nchi.                                                                                                                                                                           
Mbunge wa jimbo la Hai Mh Freeman Mbowe ni mfano mzuri wa kiongozi anayekumbuka alikotoka.Kiongozi huyu yupo mstari wa mbele kabisa kataka kutetea maslahi ya wananchi wake wa jimbo la Hai na watanzania wote kwa ujumla.Licha ya kua tu kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni amekua mfano mkubwa wa kuigwa na vijana wengi wanohitaji mabadiliko.Sio yeye tu bali wapo na viongozi wengine wengi tu kama Mh:January Makamba mbunge wa Bumbuli ambaye ni hazina kubwa kwa taifa hususani kwa chama chake cha siasa.Pia yupo Mh:James Mbatia mbunge viti maalumu jimbo la Vunjo huyu pia ni mfano mzuri wa waheshimiwa wanaokumbuka walikotoka.Kwa leo wacha tuishie na hao wachache na tutaendelea kuwafahamu wengine wengi ikiwa nipamoja na waliosahau walipotoka.Hio itajumuisha wanasiasa,wanamichezo na watu maarufu kadha wa kadha
Next
Newer Post
Previous
This is the last post.

Post a Comment

 
Top