Usajili wa kielektroniki  umeanza

Usajili wa kielektroniki Tanzania umeanza
Leo imeingia siku ya pili kwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam kujiandikisha katika daftari la kupiga kura kwa kutumia mfumo wa kieletroniki maarufu kama BVR.
Wakazi wapatao milioni tano ambao wana sifa ya kupiga kura wanalengwa
Katika zoezi hili ambalo linatarajiwa kudumu kwa siku kumi, tume ya uchaguzi ya taifa inatarajia kusajili wakazi wapatao milioni tano ambao wana sifa ya kupiga kura.
Zoezi hili linatarajiwa kudumu kwa siku kumi
Hata hivyo, wakati zoezi hilo likiendelea, tayari linaonekana kuwa kero miongoni mwa wakazi.
Vituo vingi vinadaiwa kucheleweshwa
Katika baadhi ya vituo ambao inaarifiwa kuwepo kwa ucheleweshwaji huku katika maeneo mengine kukiwa na mashine chache za uandikishaji.
Mashine zinadaiwa kuwa chache
Je umejiandikisha kupiga kura katika mfumo huo mpya wa kielektroniki?
Tusimulie yaliyokusibu

Post a Comment

 
Top