Mkutugenzi mkuu wa kampuni ya Toshiba
Mkurugenzi mkuu wa kampuni ya Toshiba akiwasili kwenye mkutano wa waandioshi wa habari
Wakuu wa kampuni ya Toshiba nchini Japan wameingia mashakani baada ya kubainika kuwa hawakua wakweli katika kutangaza faida halisi ya ambayo kiwanda hicho kilipata kwa miaka kadhaa.
Nafasi ya bwana Tanaka Hisao sasa itachukuliwa na mwenyekiti wake Masashi Muromachi.
Makamu mwenyekiti Norio Sasaki pia atajiuzulu.
Mkurugenzi mkuu wa Toshiba
Mkurugenzi mkuu wa Toshiba Bwana Hisao Tanaka akiinamisha kichwa mbele ya wanahabari
Jana jopo huru lililoteuliwa na Toshiba lilisema kuwa kiwanda hicho kilitia chumvi taarifa kwamba kilipata faida ya yen bilioni 151.8 ama dola bilioni 1.22 Kiwango hicho kilizidisha kiwango halisi kilichopatikana mara mbili.
" imebainika kuwa kumekuwa na hitilafu katika hesabu za pesa ambazo zimekua zikiendelea kwa muda mrefu , na tunaomba msamaha kwa kusababisha matatizo haya makubwa kwa wadau," ilieleza kauli ya kampuni.
Toshiba
Wakuu wa Kampuni ya Toshiba waomba msamaha kwa kudanganya juu ya faida ya kampuni hiyo
"kwasababu hii Hisao Tanaka,rais wa kampuni yetu , na Norio Sasaki, makamu mwenyekiti ... Watajiuzulu leo ." Bwana Tanaka, mwenye umri wa miaka 64, na Bwana Hisaki, mwenye umri wa miaka 66,wote walijiunga na kampuni ya Toshiba miaka ya 1970.

Post a Comment

 
Top