Waziri Mkuu wa zamani wa Tanzania, Edward Lowassa

Waziri Mkuu wa zamani wa Tanzania Edward Lowassa leo amejiunga rasmi na Umoja wa Katiba ya Wananchi, UKAWA na kuondoa hali ya sintofahamu miongoni mwa watanzania baada ya kutopata nafasi ya kuteuliwa na Chama cha mapinduzi ,CCM kupeperusha bendera ya Chama hicho katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba.
Akizungumza katika Mkutano uliowakusanya wanachama waliounda UKAWA, na waandishi wa habari, Lowassa alisema amekubali mwaliko wa kujiunga na UKAWA hususan chama cha Demokrasia na Maendeleo, CHADEMA.
Amesema baada ya kutafakari kwa kina baada ya yale yaliyotokea katika mchakato wa kumpata mgombea wa CCM mjini Dodoma kutoridhishwa nayo, ameamua kujiengua na chama hicho.
''Katiba ya CCM ilikiukwa katika mchakato wa uteuzi wa mgombea wa Urais kupitia chama cha Mapinduzi,nilifanyiwa mizengwe,majungu na habari za uongo kuhakikisha kuwa jina langu halifikishwi kwenye kamati kuu na halmashauri kuu kwa ajili ya kujadiliwa licha ya kuwa nilikuwa nikiungwa mkono na Wanachama wengi zaidi kuliko wagombea wengine'' alisema Lowassa.

Post a Comment

 
Top