Sunday, 26 July 2015

Chupi zazua kizaazaa Bungeni

 

 


Chupi zazua kihoha Bungeni

Mbunge mmoja nchini Zimbabwe alizua kizaazaa bungeni pale alitumia chupi za kina mama kusisitiza hatma ya raia masikini wa nchini hiyo ambao hawana uwezo wa kununua chupi mpya.
Katika kikao kilichokua kikipeperusha moja kwa moja kwenye runinga ya taifa, Priscilla Misihairabwi-Mushonga, wa chama cha upinzani cha Movement for Democratic Change (MDC), alitoa karatasi ya plastiki iliyokuwa na chupi hiyo. Kisha akamuuliza waziri wa fedha na sera za serikali kuhusiana na uagizwaji wa chupi kukuu ambayo anasema ni ya bei nafuu na zinasababisha madhara makubwa kwa afya ya kina mama.
''Bwana spika hebu tazama hizi chupi ninazo hapa, hizi ni mpya na hugharimu dola mbili kila moja.''

Mbunge huyo Misihairabwi-Mushonga baadaye alitimuliwa bungeni baada ya kumkabili vikali mbunge wa chama tawala cha ZANU-PF

''Hizi zilizoko mkono wangu wa kushoto ni mitumba na hugharimu dola moja kwa chupi mbili. alisema mbunge huyo
Akijibu swali hilo waziri wa fedha Patrick Chinamasa alimtania mbunge huyo Misihairabwi-Mushonga kutokana na uamuzi wake wa kubeba chupi hizo bungeni lakini amesema wizara yake inachunguza suala hilo. ''Bwana Spika, kabla sijajibu swahili hilo, naamini mheshimiwa mbunge hangelifanya kitendo kama hicho kusisitiza hoja yake'' alisema waziri huyo wa fedha.

Uchumi wa Zimbabwe umedorora kwa miaka kadhaa iliyopita

Chinamasa amesema atalishughulikia suala hilo wiki ijayo wakati atakapotoa taarifa rasmi ya serikali kuhusuiana na sera zake za kiuchumi.
Mbunge huyo Misihairabwi-Mushonga baadaye alitimuliwa bungeni baada ya kumkabili vikali mbunge wa chama tawala cha ZANU-PF ambaye alimshutumu kwa kutumia matamshi ya kibaguzi.
Uchumi wa Zimbabwe umedorora kwa muda wa miaka kadhaa iliyopita hali iliyosababisha viwango vya umasikini kupanda kutokana na idadi kubwa ya watu wasio na ajira.

Nguo kuukuu au mitumba zimefurika masoko ya nchi hiyo

Nguo kuukuu au mitumba zimefurika masoko ya nchi hiyo na mara nyingi huagizwa kutoka Mozambique na Zambia.
Nguo zingine hutengenezwa uchina huku zingine zikitoka Ulaya kama misaada.
Mwaka wa 2012 waziri wa fedha Tendai Biti alitaka serikali ya nchi hiyo kupiga marufuku uuagizaji wa chupi za mitumba akisema ni tishio kubwa kwa afya ya raia wa nchi hiyo.

No comments:

Post a Comment