Tuesday, 28 July 2015

Lowasa akihama chama cha CCM



Waziri Mkuu wa zamani wa Tanzania, Edward Lowassa

Waziri Mkuu wa zamani wa Tanzania Edward Lowassa leo amejiunga rasmi na Umoja wa Katiba ya Wananchi, UKAWA na kuondoa hali ya sintofahamu miongoni mwa watanzania baada ya kutopata nafasi ya kuteuliwa na Chama cha mapinduzi ,CCM kupeperusha bendera ya Chama hicho katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba.
Akizungumza katika Mkutano uliowakusanya wanachama waliounda UKAWA, na waandishi wa habari, Lowassa alisema amekubali mwaliko wa kujiunga na UKAWA hususan chama cha Demokrasia na Maendeleo, CHADEMA.
Amesema baada ya kutafakari kwa kina baada ya yale yaliyotokea katika mchakato wa kumpata mgombea wa CCM mjini Dodoma kutoridhishwa nayo, ameamua kujiengua na chama hicho.
''Katiba ya CCM ilikiukwa katika mchakato wa uteuzi wa mgombea wa Urais kupitia chama cha Mapinduzi,nilifanyiwa mizengwe,majungu na habari za uongo kuhakikisha kuwa jina langu halifikishwi kwenye kamati kuu na halmashauri kuu kwa ajili ya kujadiliwa licha ya kuwa nilikuwa nikiungwa mkono na Wanachama wengi zaidi kuliko wagombea wengine'' alisema Lowassa.

Sunday, 26 July 2015

14 wauawa katika shambulizi Cameroon.


 
Watu 14 wameuawa jana usiku katika shambulizi la bomu lililotekelezwa na Boko Haram

Watu 14 wameuawa jana usiku katika shambulizi la bomu lililofanyika kwenye jumba moja la starehe katika mji wa Maroua Kaskazini mwa Cameroon.
Siku chache baada ya kutokea kwa mashambulizi mawili ya bomu katika mji mkuu wa eneo hilo kulingana na habari kutoka kwa maafisa wa usalama.
Afisa mmoja wa jeshi lililopelekwa katika eneo hilo kupambana na Boko Haram ndiye aliyetoa habari hiyo kwa siri.
Shambulizi hilo lilifanyika saa mbili kasorobo jana usiku saa za Afrika Mashariki wakati mwanaume mmoja alirusha bomu ndani ya baa katika wilaya ya Ponre kulingana na afisa huyo wa jeshi ambaye hakutaka kutajwa.
Wakazi walijaribu kumfuata lakini aliwarushia grunedi kuwafukuza.
Afisa wa polisi aliyekuwa katika eneo hilo la tukio, amesema alihesabu miili 12 baada ya shambulio hilo.

Watu 25 waliuawa katika mashambulizi mengine yanayoaminika kufanywa na Boko Haram Nigeria

Mkazi mmoja wa mji huo anasema kuwa kulikuwa na mlipuko mkubwa ndipo baadaye wakajua ni baa kubwa inayoitwa"Boucan" ndiyo iliyokuwa imeshambuliwa.
Jumatano iliyopita watu 13 waliuawawa katika mashambulizi mawili yaliyotokea wakati mmoja katika soko kuu na karibu na eneo jirani.
Mashambulizi hayo yalitekelezwa na wasichana wawili waliokuwa chini ya umri wa miaka 15.
Shambulizi hilo lilikuwa la pili kwa ukubwa katika eneo hilo ndani ya siku kumi licha ya kuwa na kampeni kali za kukabili Boko Haram ambalo linaendelea kuwa tishio la usalama katika eneo la Ziwa region.
Siku ya Jumamosi watu 25 waliuawa katika mashambulizi mengine yanayoaminika kutekelezwa na wanamgambo wa Boko Haram kaskazini magharibi mwa Nigeria, huku wakaazi wengi wakilazimika kuhama makwao.

Muungano wa wanajeshi wa nchi tano kutoka Nigeria, Niger, Chad, Cameroon na Benin utatumwa kukabiliana nao

Kwa miaka miwili iliyopita kundi hilo limekuwa likifanya mashambulizi katika eneo la mpakani mbali na utekaji nyara kaskazini mwa Cameroun.
Aidha nchi hiyo ambayo ilikuwa imejitolea kuongeza jitihada za kupambana na kundi hilo haikuwa ikishambuliwa na walipuaji wa kujitolea muhanga.
Muungano wa wanajeshi wa nchi tano kutoka Nigeria, Niger, Chad, Cameroon na Benin utatumwa kukabiliana na kundi hilo linalohusiana na lile la Islamic State.
Kuwepo kwa wapiganaji hao kwa miaka sita umesababisha vifo vya watu 15,000 na tishio kubwa zaidi la usalama katika kanda hiyo.

Chupi zazua kizaazaa Bungeni

 

 


Chupi zazua kihoha Bungeni

Mbunge mmoja nchini Zimbabwe alizua kizaazaa bungeni pale alitumia chupi za kina mama kusisitiza hatma ya raia masikini wa nchini hiyo ambao hawana uwezo wa kununua chupi mpya.
Katika kikao kilichokua kikipeperusha moja kwa moja kwenye runinga ya taifa, Priscilla Misihairabwi-Mushonga, wa chama cha upinzani cha Movement for Democratic Change (MDC), alitoa karatasi ya plastiki iliyokuwa na chupi hiyo. Kisha akamuuliza waziri wa fedha na sera za serikali kuhusiana na uagizwaji wa chupi kukuu ambayo anasema ni ya bei nafuu na zinasababisha madhara makubwa kwa afya ya kina mama.
''Bwana spika hebu tazama hizi chupi ninazo hapa, hizi ni mpya na hugharimu dola mbili kila moja.''

Mbunge huyo Misihairabwi-Mushonga baadaye alitimuliwa bungeni baada ya kumkabili vikali mbunge wa chama tawala cha ZANU-PF

''Hizi zilizoko mkono wangu wa kushoto ni mitumba na hugharimu dola moja kwa chupi mbili. alisema mbunge huyo
Akijibu swali hilo waziri wa fedha Patrick Chinamasa alimtania mbunge huyo Misihairabwi-Mushonga kutokana na uamuzi wake wa kubeba chupi hizo bungeni lakini amesema wizara yake inachunguza suala hilo. ''Bwana Spika, kabla sijajibu swahili hilo, naamini mheshimiwa mbunge hangelifanya kitendo kama hicho kusisitiza hoja yake'' alisema waziri huyo wa fedha.

Uchumi wa Zimbabwe umedorora kwa miaka kadhaa iliyopita

Chinamasa amesema atalishughulikia suala hilo wiki ijayo wakati atakapotoa taarifa rasmi ya serikali kuhusuiana na sera zake za kiuchumi.
Mbunge huyo Misihairabwi-Mushonga baadaye alitimuliwa bungeni baada ya kumkabili vikali mbunge wa chama tawala cha ZANU-PF ambaye alimshutumu kwa kutumia matamshi ya kibaguzi.
Uchumi wa Zimbabwe umedorora kwa muda wa miaka kadhaa iliyopita hali iliyosababisha viwango vya umasikini kupanda kutokana na idadi kubwa ya watu wasio na ajira.

Nguo kuukuu au mitumba zimefurika masoko ya nchi hiyo

Nguo kuukuu au mitumba zimefurika masoko ya nchi hiyo na mara nyingi huagizwa kutoka Mozambique na Zambia.
Nguo zingine hutengenezwa uchina huku zingine zikitoka Ulaya kama misaada.
Mwaka wa 2012 waziri wa fedha Tendai Biti alitaka serikali ya nchi hiyo kupiga marufuku uuagizaji wa chupi za mitumba akisema ni tishio kubwa kwa afya ya raia wa nchi hiyo.

Wamaasai watakaomtumbuiza Obama


  Kundi la Olalang

Huku usalama ukiwazuia maelfu ya mashabiki wa rais wa Marekani kukutana naye ama hata kuhudhuria kongamano atakalohutubia katika ziara yake ya siku tatu mjini Nairobi Kenya, kundi la waimbaji kutoka jamii ya kimaasai imepata fursa ya kipekee.
Waimbaji hao wametunukiwa jukumu la kumtumbuiza rais Obama.
Kundi hilo la Olalang ndilo litakalomburudisha rais Obama atakapozuru Kenya leo.
Kundi hilo la Kimaasai kutoka mji wa Maasai Mara nchini Kenya limeandaa nyimbo na densi za kimaasai tayari kabisa kukonga moyo wa kiongozi mwenye nguvu zaidi duniani.
Kundi hilo linalowajumuisha wanaume na wanawake kutoka jamii ya maasai limekuwa likifanya mazoezi kwa zaidi ya miezi mitatu tangu lilipoarifiwa kuwa litamtumbuiza rais Obama.

Wanachama wa kundi hili wamevalia sare na mapambo ya kimaasai.

Wanachama wa kundi hili wamevalia sare na mapambo ya kimaasai.
Tabasamu yao inaoana na rangi nyekundu ambayo inatawala taswira ya sare yao rasmi.
Kila mmoja akiwa ni mchangamfu kutokana na burudani kali inayotarajiwa kutoka kwao.
Mkurugenzi wa kundi hilo, Gideon ole kitare, anasema kuwa wanafurahia kuchaguliwa kumpokea mgeni wa hadhi ya Rais Obama.
‘Hii ni mara yetu ya kwanza kuwa katika ngazi ya kimataifa na tunatarajia kuwa itakuwa ni fursa kubwa kuonekana na wageni kutoka nchi za nje na hata kualikwa kuandaa burudani nje ya nchi.
Hata hivyo, kundi hili ni la densi maalum kwa Rais Obama kinyume na densi za kawaida.
James Ole Kar Kar, mmoja wa waimbaji wa kundi hili, anasema kuwa wamejumuisha nyimbo na densi maalum za kimaasai kwa sababu ya rais Obama.
‘’Tumemuandalia wimbo unaoitwa ''Orkonti'' ambao ni wimbo wa kumkaribisha shujaa kama Rais Obama.’’
‘’Wimbo huo ni wa kumpa nguvu shujaa ili aweze kuwa na uwezo wa kufanya mambo muhimu.’’ Aliongeza

Sylvia Lesaloi,anasema watampokea rais Obama kama 'mtoto anayerejea nyumbani '

Kwa upande wake, Sylvia Lesaloi, mmoja wa viongozi wa kundi hili, anasema kuwa yeye pamoja na kina mama wenzake katika kundi hilo, watampokea Rais Obama kama mtoto anayerejea nyumbani baada ya kuondoka kwa kipindi kirefu.
‘’Rais Obama ni mtoto wetu, tunafurahi ametutembelea safari hii na pia tungependa awe akitutembelea hata atakapomaliza muhula wake kama rais wa Marekani.''
Aidha Bi. Sylvia ana ujumbe moja tu kwa Rais Obama.
'' iwapo tutapata fursa ya kuwasilisha ombi kwa Rais Obama, Tutamuomba atusaidie kuhifadhi msitu wa Mau ambao unatishiwa na unyakuzi na uharibifu wa kimazingira.''
''Tuanomba atausaidie ili tuweze kuulinda msitu huo wa Mau’’.
Msitu wa Mau ni msitu mkubwa wa kiasili na ambao ndio chanzo cha mito mingi inayotiririka kupitia mbuga kuu ya wanyama ya Maasai Mara na pia mito inayotiririka hadi kwenye ziwa Victoria.
Hata hivyo katika miaka ya hivi punde viongozi wa kuu katika serikali zilizopita nchini Kenya walinyakua vipande vikubwa vya msitu na kukata miti.

Wamaasai watakaomtumbuiza Obama wakiwa na mwandishi wetu Abdi Noor

Athari yake imekuwa kupunguka kwa kiwango cha mvua katika maeneo karibu na msitu huo.
Eneo la Maasai Mara, makao ya kundi hili, ni eneo alilozuru rais Obama alipowasili nchini Kenya mara ya mwisho.
Eneo hilo ni mojawapo ya maeneo yanayowavutia watalii wengi wa kigeni nchini Kenya.
Densi na nyimbo za kimasaai zimekuwa na mvuto mkubwa kwa watalii nchini Kenya lakini wanachama wa kundi hili wanasema kuwa Obama sio mtalii wa kawaida ni shujaa wa hapa nchini Kenya.

ZIARA YA RAIS OBAMA KENYA YAKAMILIKA

RAIS WA MAREKANI BARRACK OBAMA AMEKAMILISHA ZIARA YAKE YA SIKU TATU NCHINI KENYA AMBAPO ALIFUNGUA KONGAMANO LA KIBIASHARA AKAWAHUTUBIA WAKENYA KATIKA UWANJA WA KASARANI NA BAADAYE KUZUNGUMZA NA VIONGOZI WA MASHIRIKA YA KIJAMII KATIKA CHUO KIKUU CHA KENYATTA

Obama Kwaheri

16.18pm:Ndege ya rais Obama yaondoka katika uwanja wa Jomo Kenyatta

Obama amuaga Uhuru

16.13pm:Rais Obama awasili katika uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta Jijini Nairobi na kulakiwa na rais Uhuru Kenyatta tayari kuondoka
16.10pm:Ndege iliombeba rais wa Marekani Barrack Obama imewasili katika uwanja wa ndege wa JKIA jijini Nairobi.

Mama sarah Obama tayari kumuaga rais Obama

15.47pm:Rais Obama amekamilisha ziara yake nchini Kenya na sasa anaelekea nchini Ethiopia kwa ziara ya siku mbili ambako anatarajiwa kuzungumza kuhusu maendeleo ya eneo hili.
15.46pm:Msafara wa rais Uhuru Kenyatta umewasili katika uwanja wa Jomo Kenyatta tayari kumuaga rais Obama aliyewasili nchini siku ya ijumaa.

Uwanja wa ndege

15.45pm:Matayarisho yote ya kumuaga rais Obama katika uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta yamekamilika huku zulia jekundu likiwekwa.
15.43pm:Msafara wa Rais Uhuru Kenyatta waonekana ukielekea katika uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta kumuaga rais Obama.
14.55pm:Obama amaliza mkutano wake na makundi ya kijamii katika chuo kikuu cha Kenyatta.

Obama

14.51pm:Tutahakikisha katika mazungumzo yote na serikali kwamba yale yanayozungumzwa yanaangaziwa na iwapo kuna kundi linalokandamizwa basi tutatoa sauti yetu.Viongozi wengi wanapendelea sa na Marekani kuingilia kati wakati hawako katika mamlaka,lakini punde wanapoingia katika mamlaka
14.49pm:Obama:Iwapo kuna sheria ambazo zinatoa fursa kwa jamii kujieleza huchangia ukuwaji wa kimaendeleo.Tutaziangazia sheria zinazojaribu kuwazuia watu wengine kuzungumza.SWala la kigadi halifai kuchukuliwa kuyazima makundi ya kijamii ambayo ni halali.
14.34pm:Sisters Without Borders-Serikali inafaa kuwashirikisha wanawake katika harakati za kukabiliana na utovu wa usalama.Licha ya harakati zetu katika swala hilo serikali bado haijatilia mkazo swala la thuluthi moja ya wanawake katika kila sekta.

Obama

14.32pm:SUPKEM-Maafisa wa serikali kama vile walimu wametoroka katika maeneo ya kaskazini mwa Kenya na hivyobasi kuathiri elimu katika eneo hilo miongoni mwa vijana wengi.
14:29pm:SUPKEM-Viongozi wa Kiislamu pia wameshirikishwa katika kukabiliana na ugadi pamoja na ukandamizaji ikiwemo ukosefu wa vitambulisho kwa vijana wa kiislamu.
14:26pm:SUPKEM-Hassan Olenaado:Tumezungumza na serikali kuhusu kuanza mikutano ya kukabiliana na itikadi kali

Obama

14.24pm:Ugaidi:Alilirejelea swala ya kukabiliana na ufisadi,akisema ni muhimu kubadilisha fikira za raia kuhusu vita dhidi ya ugaidi.Amsema kuwa huwezi kukabiliana na ufisadi kwa kutumia nguvu pekee.
14.05pm:Habari njema nchini Kenya ni kwamba kuna katiba mpya ambayo inatoa mwongozo.Baadaye alifungua mjadala wazi katika kikao hicho.
14.02pm:Makundi ya kijamii yalijitokeza baada ya raia kujitokeza na kuanza kuzungumzia maswala yanayowaathiri
13.50pm:Obama awasili katika chuo kikuu cha Kenyatta na sasa anawahutubia viongozi wa makundi ya kijamii

Chuo kikuu cha Kenyatta University

13.00pm:Chuo Kikuu cha Kenyatta Jijini Nairobi
12.42pm:Obama amaliza hotuba yake kwa kusema 'Thank you Asante sana'
12.41pm:Amesema kuwa vijana wamemfanya yeye kujisikia nyumbani.

Obama

12.37pm:Ametoa changamoto kwa vijana kuchukua fursa iliopo ili kuiendeleza jamii huku akiongezea kuwa ana hakika kwamba kenya inaelekea katika ufanisi mkubwa
12:35pm:Amewataka wakenya kutokubali kugawanywa katika misingi ya kikabila na kidini.
12:33pm:Amesema kuwa Marekani itashirikiana kwa hali na mali na kenya kukabiliana na tatizo la ugiadi.'Magaidi ni waoga ndio maana hupendelea kutafuta makundi madogo madogo ya kijamii na kujaribu kuyagawanya''.Amesisistiza kuwa ugaid ni sharti ukabiliwe kwa hali yoyote.
12.32pm:Amesema kuwa ni sharti wanawake wapewe nafasi sawa katika jamii.'Udhalilishaji wa wanawake ni utamaduni ambao umekuwa tangu zamani lakini sasa hauna nafasi katika maisha ya sasa .Wanawake na wasichana ni sharti waelemishwa,Amesema kuwa kuna ufanisi mkubwa katika jamii ambayo imewaelemisha wanawake wake.Tuwape wasichana wetu elimu.Tunapowaelimisha wanawake tunawapatia nguvu kuzaa watoto walioelimika.

Obama kasarani

12.27pm:Amesema kuwa Marekani inashirikiana na Kenya kupitia uwekezaji wa vijana nchini.Amesema kuwa kila taifa lina utamaduni wake,lakini akaongeza kwamba tamaduni nyengine zimepitwa na wakati.Unyanyasaji wa kijinsia ni tamaduni iliopo lakini ni lazima zibadilishwe.zinawarudisha nyuma.
12.25pm:Amasema kuwa harakati za kukabiliana na ufisadi lazima zianze kuanza juu na kwamba sheria za kukabiliana na janga hilo ni sharti ziwekwe,huku akiwataka wananchi kusimama kidete na kukataa ufisadi.
12.23pm:'Ufisadi ndio janga linalozuia mataifa mengi kupiga hatua'.Amesisitiza kuwa iwapo Ufisadi hautakabiliwa vilivyo utaathiri maendeleo ya taifa kwa jumla

Obama-kasarani

12.20pm:'Kwa ushirikiano wetu kuimarika ni sharti tuwe na taasisi zilizo imara katika uongozi wa taifa hili kwa lengo la kuimarisha demokrasia'.Amesema kuwa mara nyengine demokrasia huonekana kupendelea upande mmoja lakini sivyo akasisitiza.Amesema kuwa wanasiasa huwa na misimamo tofauti na hutarajia demokrasia itawapendelea na wasipopendelewa hulalama.
12.17pm:Amesema kuwa Marekani ni mshirika wa karibu na rafiki mkubwa wa Marekani na hivyobasi itaendelea na ushirikiano huo kupitia kuhakikisha kuwa kuna uongozi mzuri nchini Kenya.

Obama

12.16pm:Ugaidi ni swala jingine ambalo Obama anasema kuwa limerudisha nyuma maendeleo na kutoa heshima zake kwa wale ambao wamepoteza maisha yao katika kukabiliana na janga hilo pamoja na wale walioathirika.
12.15pm:'Siasa za kikabila na za kibaguzi hazina mwelekeo na hazifai kuendelezwa',alisema Obama
12.14pm:Ufisadi-amesema kuwa unafaa kukabiliwa kwa njia mbali mbali kwa kuwa unawadhulumu wakenya wa kawaida pato lao la kila siku.

Obama na Rais Obama

12.12pm:Alitoa sifa kwa marehemu Wangari Maathai kwa jitihada zake na ukakamavu wa kupigamnia demokrasia.
12.11pm:Amesema kuwa wakenya walikataa kugawanywa katika misingi ya kikabila huku sauti za viongozi na makundi ya kijamii yakisababisha kupitishwa kwa katiba mpya

Ghasia za baada ya uchaguzi nchini Kenya

12.10pm:Alizungumza kuhusu vita vya baada ya uchaguzi wa mwaka 2007 ambapo nusra viangamize taifa la Kenya.
12.09pm:Uwezo wa vijana na maendeleo yaliopigwa na kenya ni fursa nzuri kwa vijana kujiendeleza wakati wowote.
12.06pm:Babu yangu alikuwa mpishi wa wakoloni.Obama alieleza vile alivyoweza kupata elimu.
12.04pm:'katika uwanja wa ndege mwanamke mmoja aliona jina langu na kuniuliza iwapo ninahusiana na Mtu anayemjua kwa jina Barrack Obama,na hapo ndipo nilijua kuwa jina hilo ni muhimu'

Obama

12.03pm.Obama anasema kuwa alipozuru kenya kwa mara ya kwanza alikula ugali na sukuma na pia alikuwa akilala katika kiti katika nyumba ya dadaake Auma.

Obama akiwasili

12.03pm:'Nakumbuka nilipokuja miaka 30 iliopita nilipoteza mzigo wangu katika uwanja wa ndege wa Jomo kenyatta ,lakini hilo haliwezi kufanyika katika Airforce one'.alisema Obama

Rais Barrack Obama na UHuru Kenyatta

12.01pm:Obama aingia katika jukwaa na kuwasalimia wakenya Habari zenu,wakenya mupo.Nafurahi kuwa wakenya kwa kuwa rais wa kwanza kutembelea kenya.Na pia kuwa mtu wa kwanza kutoka kenya kuwa rais wa Marekani,.
12.00pm:Auma amkaribisha Obama

The beast

11.58am:Amewachekesha wengi aliposema kuwa nduguye Barrack ambaye alimchukua katika uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta kwa gari aina ya Beattle takriban miaka 30 iliopita amerudisha hisani yake alipombeba ndani ya gari la the Beast wakati alipowasili.
11.56am:Auma amewakumbusha wakenya kwamba rais Obama yuko hapa kikazi licha ya kuwa mwana wa kenya.
11.53am:Awahutubia wakenya kuhusu dhifa ya hapo jana ambapo anasema kuwa rais huyo wa Marekani alikula vyakula vya aina mbali mbali vya kienyeji licha ya kukaa Marekani kwa muda mrefu.

Auma na dadaake bi Auma Obama

11.52am:Dadaake Rais Obama Auma Obama amepanda katika jukwaa kwa sasa
11.30am: Obama-Rais Barrack Obama wa Marekani pia amedaiwa kufika katika maeneo ya uwanja wa kasarani jijini Nairobi na wakati wowote kuanzia sasa atakaribishwa na mwenyeji wake Uhuru Kenyatta ndani ya Ukumbi huo.
11.25am:Uhuru awasili Ukumbini

Uhuru Kenyatta

Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya amewasili katika ukumbi wa Kasarani
11.10am:Ukumbi wa Kasarani

Ukumbi wa kasarani

Ukumbi wa Kasarani ambapo rais Barrack Obama wa Marekani na mwenyeji wake wa Kenya Uhuru Kenyatta wanapaswa kuwahutubia Wakenya tayari umejaa mamia ya wageni waalikwa wakiwasubiri viongozi hao wawili.Tayari viongozi mbali mbali wakiwemo wale wa Upinzani wamewasili katika eneo hilo.
11.05am:Usalama Kasarani

Usalama K
Usalama

Usalama umeimarishwa katika uwanja wa Kasarani,ambalo ndio eneo ambalo rais Barrack Obama wa Kenya anatarajiwa kuwahutubia Wakenya
11.01am:Obama akicheza densi

Rais Obama

Rais wa marekani Barrack Obama siku ya jumamosi usiku alijiunga na mwenyeji wake Uhuru Kenyatta katika chakula cha usiku na baadaye kucheza densi katika ikulu ya rais jijini Nairobi.